GET /api/v0.1/hansard/entries/800259/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 800259,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800259/?format=api",
    "text_counter": 79,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono Hoja hii iliyoletwa na Sen. Kihika kuhusu janga la mafuriko lililotokea sehemu ya Solai. Nawapa pole zangu walioathirika na kuunga mkono Kamati ambayo imechaguliwa kwenda kuchunguza tukio hilo. Mambo ya Solai yalikuwa magumu sana na ya kusikitisha. Nawatangazia ya kwamba sehemu nyingi nchini mvua imesita wakati huu. Hata hivyo, kuna mafuriko mengi katika Kaunti ya Tana River tangu juzi kuliko wakati ule w amwanzo. Jambo hili linasikitisha sana. Maji yanayo beba watu sehemu hiyo ni yale yanayo achiliwa kwa makusudi kwenda kuathiri watu wa Kaunti ya Tana River. Bw. Mhe. Spika, mabwawa ambayo yanatumiwa kuzalisha umeme katika sehemu ya juu ya Mto Tana kama vile Masinga, Kindaruma na Kiambere yanaendelea kuachilia maji kwa wingi sana wakati huu. Ni ajabu sana kuwa wakati mvua imesita, maji yanabeba watu Tana River. Wakati huu ninapoongea, sehemu ya Tana Delta imezama kabisa. Miji yote iko nusu mlingoti ndani ya maji, majumba yote yamesombwa kuanzia sehemu ya Kipini mahali Mto Tana unaunganika na Bahari Hindi. Sehemu ya Kikomo, Kipao, Otole na Handaraku zote zimezama. Watu hao walipata nafuu wiki jana na w kurudi makwao, na mara ya nne wameondolewa tena. Wakati huu wanatangaziwa waende sehemu za nyanda za juu. Hakuna nyanda za juu upande huo kwa sababu yote ni sehemu ya maji. Bw. Mhe. Spika, wakati huu, watoto hawaendi shule. Ninaweza kukueleza yale Kamati hii inaweza kwenda kuandika kwa sababu niko na taarifa hiyo tayari. Watu upande huo wanaugua malaria kwa wingi, kuumwa na tumbo, kuendesha tumbo na maradhi ya ngozi yaliyoletwa na maji. Hali ni ya kusikitisha sana sehemu hiyo. Dunia yote na Kenya inajua kuwa Kaunti ya Tana River ndiyo sehemu ambayo imeathirika zaidi. Maji yote ambayo yananyesha sehemu za juu ya mlima Kenya, yanafuata mto huo na kuelekea Kaunti ya Tana River. Seneta wa Kaunti ya Tana River anafaa kuwa katika Kamati ambayo itaangalia maafa ya maji. Hii ni kwa sababu sehemu hiyo imeathirika na nyote mnajua. Hata nchi za nje zinajua kuwa sehemu hiyo imefurika na nyumba zote ziko nusu mlingoti ndani ya maji. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}