GET /api/v0.1/hansard/entries/800261/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 800261,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800261/?format=api",
"text_counter": 81,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kama kuna historia mbaya ya kuandikwa kuhusu mathara ya maji, Kaunti ya Tana River iko mstari wa mbele. Sioni sababu ya Seneta wa Kaunti ya Tana River kukosa katika Kamati ya kuangalia majanga yanayoletwa na maji hasa wakati huu. Ninaunga mkono Hoja ya Seneta wetu mpendwa, Sen. Kihika, na singependa kupoteza wakati kwa kuleta Hoja ambayo ni sawa na Hoja hii ambayo iko mbele yetu. Ningependa kuunganisha Hoja hii na mambo ya Kaunti ya Tana River. Hoja hii inahusu mkasa wa Solai, lakini nikileta Hoja ingine kesho kuhusu kuundwa kwa Kamati maalum ya kuangalia maafa ya maji, tutakua tunafanya kazi ambayo inafanana kwa wakati moja. Ili tutumie wakati vizuri na kufanya kazi nzuri, ningependa kuunganisha Hoja yangu pamoja na Hoja hii ili Kamati hii iweze kwenda Solai na Kaunti ya Tana River. Katika hali hiyo nimeshatembea Kaunti ya Tana River na Kamati ya Seneti ambayo inaangalia mambo ya usalama. Tulienda kule na Sen. Haji, Sen. Sakaja, Seneta wa Lamu, Sen. Pareno na Sen. Wetangula. Tulisafiri kwa ndege na kuangalia vile miji ilivyoathirika katika Kaunti ya Tana River. Huwezi kuamini yale tuliyaona na mashahidi wako hapa. Nyumba katika miji zaidi ya 30 ziko ndani ya maji nusu mlingoti. Ng’ombe na mbuzi wote wamesombwa hadi Bahari Hindi. Vile vile kuna watu ambao wamesombwa na mali zao zote. Ninavyoongea, watu wanaishi katika hema ambazo zimepelekwa na Shirika la Msalaba Mwekundu. Bw. Spika, mambo ya Kaunti ya Tana River ni zaidi ya vile tunavyoongea hapa na yale yanayoandikwa kwenye magazeti. Hali kule ni ya kutatanisha. Watu wengi walifariki kule Solai na wakazikwa, lakini ninawatangazia kwamba watu kule Tana River wanendelea kusombwa na maji na kuzikwa kila kukicha. Hata jana, kuna kijana aliyesombwa na maji akienda shule. Kwa hivyo hali hii itaendelea kule Tana River kwa sababu wasimamizi wa mabwawa ya maji ambayo yanazalisha umeme upande wa juu wa Mto Tana bado wanaendelea kuwachilia maji kwa kusudi bila kujali haya maji yanaenda wapi. Hakuna mtu wa Tana River ambaye ameajiriwa na Kenya Electricity Generating Company (KenGen), licha ya maafa mengi ambayo yanaletwa kule. Isitoshe, sehemu nyingi katika Kaunti ya Tana River hazina umeme. Watu wengi wanaishi katika hali duni. Ningependa kuomba kwamba Seneta wa Tana River ajumuishwe katika Kamati hii ili niweze kwenda na Kamati hii kule Kaunti ya Tana River baada ya kutembelea Solai ili niwaonyeshe hali halisi ilivyo na yale maafa ambayo yanaletwa. Maafa ya Solai yametokea mara moja lakini yale ya Tana River yalitokea hapo mbeleni na yataendelea kutokea kwa sababu mabwawa ambayo yako juu na yanazalisha umeme; bado yatakuwa hapo na mvua itaendelea kunyesha. Iwapo mvua itaendelea kunyesha na mabwawa yatakuwa hapo, maafa haya yatatokea hata miaka zijazo. Hali hiyo inafaa kuchunguzwa na ripoti halisi iweze kuletwa katika Seneti hii. Tunafaa kufanya mambo ambayo tunaweza kufanya ili tuepukane na hali kama hii katika siku zijazo. Bw. Spika, vile nilisema hapo awali, haifai kuletwa kwa Hoja tofauti kuhusu maji kila wakati. Kwa hivyo ningependelea Hoja hii ihusishe pia maafa katika Kaunti ya Tana River. Ningependa hasa wewe kama Spika wetu uweze kuangalia jinsi ambavyo Hoja hii inaweza kuhusisha Kaunti ya Tana River. Pia, sio siri ya kwamba Kaunti ya Tana River imeathirika zaidi na maji yote ambayo yanatoka sehemu za juu. Hata maji ya mvua inayonyesha hapa Nairobi yanaelekea sehemu ya Tana River. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}