GET /api/v0.1/hansard/entries/800286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 800286,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800286/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya mkasa wa Solai ambayo imeletwa na Seneta wa Kaunti ya Nakuru; Sen. Kihika. Kwanza, ningechukua fursa hii kutuma rambirambi zangu kwa mara nyingine tena kwa watu wa Nakuru kwa janga hilo lililowapata. Ninawaombea Mungu wale ambao Mwenyezi Mungu aliwachukua na aweke roho zao mahali pema peponi. Vile vile, ningependa pia kuchukua fursa hii kutuma rambirambi zangu kwa watu wa Kaunti ya Tana River ambao wamepata mkasa wa mafuriko na pia sehemu zingine zote za nchi ya Kenya ambazo kuna janga la mafuriko kwa sasa. Kwa hakika, majanga kama haya siyo ya kwanza nchini Kenya. Katika mwaka wa 1993, kulikuwa na janga kubwa la kwanza kabisa la feri ya Mtongwe ambapo zaidi ya watu 200 walifariki dunia. Wakati huo feri ilikuwa ni mali ya Serikali. Mpaka sasa, Serikali bado haijawalipa ridhaa wale ambao walipoteza maisha yao na wale ambao waliathirika na mkasa ule wa feri kuzama. Kwa hivyo, Mswada huu umekuja wakati mwafaka kabisa kwa sababu wakati wa sasa, Bunge linataka kuchukua hatua kali ili kuhakikisha kwamba mikasa kama hii ikitokea wakati mwengine, wale ambao wameathirika wanalipwa ridhaa ili iwe funzo kwa wengine. Bw. Naibu Spika, tukiangalia mikasa mingine kama vile Kyanguli, Sachangwan na pia maajuzi hapa, mkasa wa eneo la Pipeline wakati “pipe” ya mafuta ilipopasuka na kukatokea moto na watu wengi kupoteza maisha yao. Hata hivyo, mpaka sasa bado Kenya Pipeline Company haijaweza kuwalipa ridhaa."
}