GET /api/v0.1/hansard/entries/800290/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 800290,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800290/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Ndio, ni mfereji. Asante Bw. Naibu Spika. Mifereji ya mafuta ilipopasuka, mpaka leo wale ambao waliathirika bado hawajalipwa ridhaa. Kwa hivyo, imekuwa ni mwelekeo kwamba janga linatokea, watu wanaomboleza siku mbili, wanatoa hotuba kali kali, lakini baada ya hapo, inakuwa ni jambo la kawaida. Kwa upande mwingine, tunaona kwamba janga la ufisadi ni kubwa zaidi. Hii ni kwa sababu zile pesa ambazo zingekwenda kwa matibabu ya watu wote ambao hawajiwezi na kusaidia wazee wale wanaolipwa ruzuku na Serikali, zote zinafujwa kwa sababu ya ufisadi. Bw. Naibu Spika, kwa hivyo, tungeomba kwamba Serikali ichukulie majanga kama haya hatua kali zaidi kuliko vile wanavyofanya kwa sasa. Hii ni kwa sababu, baada ya Serikali kutuma ujumbe na kusema kwamba, “tunasisitiza kwamba swala kama lile halitarudiwa” lakini tunaona mikasa kama hii inaenda ikirudiwa kila mwaka. Sababu ni kwamba hatuna msimamo thabiti kuhusiana na vile tunavyokabiliana na majanga kama haya. Leo Tana River imekuwa ni kama wimbo. Kila siku tunazungumuzia Tana River na imekuwa ni Kaunti ambayo inapelekewa misaaada ya chakula kila mwezi. Hii ni kwa sababu ya majanga ya mvua na mafuriko ambayo yanakabili watu wa Tana River. Bw. Naibu Spika, ningependa pia kuunga mkono maelezo yaliyotolewa na ‘Super Senator’ wa Kaunti ya Nairobi, Sen. Sakaja."
}