GET /api/v0.1/hansard/entries/800301/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 800301,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800301/?format=api",
    "text_counter": 121,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "sana katika sehemu zile za makazi duni. Hii ni kwa sababu wengine wanashindwa kuishi na uja uzito ambao umetokana na ubakaji na hata labda ni wa familia. Kwa hivyo, ni wakati sasa mwafaka tuchore mstari tuseme kwamba yale yaliopita yashapita lakini kuanzia sasa kuenda mbele, lazima Sheria ifanye kazi yake kulingana na vile inavyotakikana. Na inamanisha kwamba, lazima tupeleke rasilmali za kutosha katika kaunti zetu ili kuhakikisha kwamba kitengo cha usalama katika hizi kaunti kinapewa fedha za kutosha. Hatua hii itahakikisha kwamba kuna vituo vya polisi vya kutosha ili polisi waweze kufukia sehemu zote kwa urahisi wakati wanapohitajika na wananchi ambao wako katika majanga tofauti tofauti. Bw. Naibu Spika, pia ningependa kuunga mkono yale majina ya Maseneta ambao wamependekezwa kuhudumu katika hii kamati maalum ya kuchunguza swala la Solai. Ninaona kwamba ni watenda kazi na wataleta ripoti ambayo itasaidia nchi hii kuenda mbele kutokana na mikasa kama hiyo. Bila ya kuongeza mengi, ninaunga mkono Hoja hii. Asante."
}