GET /api/v0.1/hansard/entries/800303/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 800303,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800303/?format=api",
"text_counter": 123,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana Bw. Naibu Spika. Mimi ninasimama kuunga mkono Hoja hii. Kwanza kabisa, ninamshukuru Seneta wa Kaunti ya Nakuru, Sen. Kihika, kwa kuleta Hoja hii. Ninasema tena, pole kwa wale waliopatwa na janga hili pale Solai, Nakuru. Kwanza ningependa kusema ya kwamba, itakuwa ni vizuri kama vile Spika alivyosoma akatuambia kwamba tunaweza kuongeza majina. Kwangu itakuwa ni kosa kama tutapitisha haya majina bila kumwongeza Seneta wa kutoka Kaunti ya Tana River. Hii ni kwa sababu, ukiongea kuhusu mambo ya mvua kunyesha na watu kubebwa hata na maji, yeye mwenyewe anauzoefu, anaujuzi na watu wake wamekuwa wakikumbwa na hilo janga mwaka nenda mwaka rudi."
}