GET /api/v0.1/hansard/entries/800309/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 800309,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800309/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo inamaanisha kuwa ikiwa kuna mabwawa saba na lile ambalo lina leseni ndilo lilisomba watu, ni heri hakungelikuwa na leseni, pengine watu hawangesombwa na maji. Idara hii imezembea kazini. Ni dhahiri kwamba ufisadi umekita mizizi kwa kuwa wafanyikazi wa zile idara hawafanyi kazi vile wanapaswa kufanya. Kwa hivyo ni vizuri sisi tuwe tunawaangalia na kila mtu aliye hapa nchini afanye kazi ile ambayo anapaswa kufanya. Jambo la pili ambalo wenzangu wamelitaja, inaonekana ya kwamba sisi huwa tunaongea jambo likitendeka. Watu wanaongea halafu baadaye wanasema, maneno haya yamekwisha. Inakuwa vile Mswahili alivyosema, “yaliyopita si ndwele tugange yajayo.” Lakini nasema kwamba yaliyopita tunapaswa tuyagange kwa sababu kama wataka kwenda mbele ni mpaka uangalie nyuma mahali umetoka. Inaonekana ya kwamba unaweza kuilinganisha nchi yetu ya Kenya na matukio katika kitabu cha Shamba laWanyama . Kuna watu ambao ni muhimu zaidi kushinda wale wengine kwa sababu janga likitokea maneno tu yanazungumzwa; watu wanaambiwa pole na hakuna chochote kinachofanyika. Twasema kwamba wale watu wa kutoka pale Solai wanapaswa kufidiwa ipasavyo kwa sababu nyumba, mifugo na mimea yao ilisombwa na maji. Sasa ni walala hoi. Inaonyesha kwamba kuna wala nyama na wala nyasi; walala hoi na wale ambao ---"
}