GET /api/v0.1/hansard/entries/800312/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 800312,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800312/?format=api",
"text_counter": 132,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Kwa hivyo ni vizuri sisi sote tufuate sheria. Sheria ya Kenya ni dhahiri kabisa. Tunapaswa kuishi kama Wakenya kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na tuzifuate ipasavyo. Ninaunga mkono Hoja hii. Hii kamati ambayo tumeteua siku ya leo ifanye kazi yake na wafuatilie vizuri kisa na maana ya jambo hili kutendeka. Kusisemekane huyu ni muungwana ambaye ni mmiliki wa mabwawa. Mkifika pale anapaswa kuulizwa maswali na ajibu vililvyo ili ijulikane wazi asiwe yeye maisha yake ni mazuri zaidi kushinda wale wengine. Inasemekana kwamba kwa sababu ana yale mabwawa anaajiri vijana wawili kazi, anajenga shule na hospitali. Hospitali tutazitengeneza za nini ikiwa watu wote watakuwa wamekufa? Shule ni ya nini ikiwa watu wote watakuwa wamesombwa na maji? Itakuwa ni bure na haina haja yoyote. Kwa hivyo tukubaliane na wale watakaotuwakilisha pale kama kamati waonyeshe ule uadilifu wetu kama Seneti kwa sababu sisi sote tujuavyo ni Waheshimiwa, watu waliomakinika na watu ambao wataangalia haya maneno kwa njia ifaayo. Tukifanya hivyo, jambo lolote likitendeka hapa, Seneti ikichunguza iweke jambo la kudumu – mambo ambayo tutakuwatukiyafuatilia. Tusiwe watu ambao kazi yao ni kukimbia wakati jambo limetendeka. Tunapaswa tuzuie kwa sababu Mswahili alisema ni bora kuzuia kulika kuponya. Asante sana Bw. Naibu Spika."
}