GET /api/v0.1/hansard/entries/800336/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 800336,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800336/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "nilipokuwa nje ya nchi, lakini kama ningekuwa, kwa hakika ningefika kwa sababu mbili. Moja, kwa sababu nafahamu kwamba niko hapa kuwakilisha kina mama. Niko na hakika kwamba mkasa ule uliwausa sana mama na watoto, ikiwa wao ndio nawaangalia sana. Japokuwa naangalia watu wote, lakini namwangalia mama kwa undani sana. Vile vile, nasimamia watu masikini, kwa sababu nimesimama hapa katika Seneti ilhali nimetoka katika jamii maskini, na najua umaskini unauma vipi. Bw. Naibu Spika, najua kwamba kuna matajiri wanaojenga kulingana na utajiri wao, na wanatafuta mahali pazuri kulingana na pesa walizonazo. Lakini vile vibanda vidogo vilvyokuwa pale, ndio vilivyokuwa mali ya wale masikini. Watu hawa wametumia wakati wao na maisha yao yote kuvitafuta, japokuwa vilikuwa vibanda vya namna gani; vilikuwa ndio uwezo wao wote. Katika Biblia, kuna mtu mmoja aliyetoa sadaka ndogo sana, na wanafunzi wakasema “huyu ametoa sadaka ndogo.” Lakini Yesu akasema “huyu ametoa kile alichokuwa nacho chote.” Kwa hivyo, kwa wale masikini, vile vibanda walivyokuwa navyo vilikuwa ndio mali yao yote na hakuna fidia ambayo inaweza kukidhi ile hasara waliyoipata. Hakuna pesa wanazoweza kupewa zinazoweza kufidia uhai wa wale waliokufa isipokuwa tu ni kuwalipa ili wale waliobakia waanze maisha upya. Lakini mwanadamu hawezi kulipika kwa sababu thamani yake na uhai wake hauwezi kuulipa. Lakini kwa sababu ni lazima tuhifadhiane na kusaidiana, ndio maana twaiomba serikali – hata sio kuiomba - twataka iwalipe fidia. Serikali inafaa ilipe pale mahali imeingilia, na vile vile huyo mtu mwenye hayo mabwawa kuna mahali pia anaingilia. Bw. Naibu Spika, shida hii haijaanza huko peke yake; shida hizi ziko Kenya mzima. Nitazungumzia sasa masuala ya Kilifi pia. Wahenga walisema “palipo na mwanzo pana mwisho” ama “marefu hayakosi ncha.” Mito hii huanzia juu, lakini miteremko yake huwa chini. Nasi, kwa bahati nzuri au mbaya, ikatokea kwamba ni wakazi wa kule chini ambako mafuriko ama maji huteremkia. Sasa, maji haya yakiteremka, huja kule pwani; na yakija, sana sana yanaumiza watu wa Tana River na Kilifi. Nikiwa natoka Kaunti ya Kilifi, hivi sasa ninavyozungumza, kama kuna watu waliangalia mtandao wa Facebook, Jumamosi niliweka habari kwamba kuna watu waliokuwa wamebebwa na maji ya Mto Galana, nikaenda katika mazishi yao. Vile vile, kuna mto Sabaki na saa hii ukienda huko chini, utakuta hakuna watu kwa sababu wamehama; wanaishi katika mashule. Kuna mashule ambayo saa hii yamefungwa kwa sababu wale watu ambao walikuwa kule chini wanakaa humo. Hivi sasa, hakuna watoto wanaoenda shule kwa sababu shule zimefungwa. Kule Pwani, sisi tumekuwa watu wa kuomba omba kila mwaka, kisa na sababu ni mafuriko. Twalia kwa kuwa hakuna mvua, lakini kila mwaka hakuna siku tutakosa mvua Kenya hii. Lakini mvua ikinyesha, hata kama haitanyesha kule kwetu, maji huja na hubeba watu, kwa sababu itanyesha huku juu na itateremka kule chini. Kwa hivyo, kunyeshe ama kusinyeshe, kule kwetu watu watakufa hivyo hivyo. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, janga hili halijaanza jana, juzi wala leo; ni la kitambo. Kuna mahali fulani kuna utepetevu; kuna watu ambao hawafanyi zile kazi ambazo wanapaswa kufanya. Kidole changu kinaelekeza sehemu mbili; Serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti. Serikali za kaunti ndizo zinajua hasa ni nini kinachoendelea pale chini mashinani. Tulipoletewa ugatuzi, tulifikiria kuna mambo mengine kama haya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}