GET /api/v0.1/hansard/entries/800338/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 800338,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800338/?format=api",
    "text_counter": 158,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ambayo hayatatokea tena. Lakini mpaka sasa, mafuriko yanatuumiza kule kwetu kwa sababu kuna watu ambao hawafanyi kazi vile wanavyopaswa kufanya. Naungana na wenzangu waliosema kuwe na sheria kali; sijui sheria itakuwa na ukali gani. Kama ni kutunga sharia nzuri nzuri, kama Wapwani sio namba moja ama sio wa kwanza, basi labda wa pili. Lakini je, twazifuata? Kiongozi mzuri ama meneja mzuri ni yule ambaye akipeana kazi, halafu huifuatilia. Sisi twatunga sheria vizuri, lakini baadaye mfuatilio hakuna. Watu wanatembea tembea kule njiani, hawafanyi kazi zao na hakuna anayewauliza kwa nini wanafanya hivi. Ningeomba, kama twasema hiki hakifai, iwe hakifai; lakini sio baadaye kikitengenezwa kiwe chafaa. Kama hakifai, hakifai! Jambo la kwanza la kufanya ili mambo kama haya yasitokee tena ni kuwa naunga mkono kwamba Kamati iliyochaguliwa iendelee. Lakini vile vile, kuwe na mfuatilio. Kama ni watu kulipwa, walipwe. Wale ambao wako kule na hawana makwao, wamewekwa katika mashule, wao pia ni binaadamu. Tumechoka kuomba omba sisi watu wa Mombasa; kila siku twaambiwa kwamba hatulimi. Twalima jamani! Lakini mvua ikinyesha kama hivi, yabeba chakula chote; mahindi yabebwa na kila kitu chabebwa, halafu twabaki vile vile, tukiomba omba. Hivi sasa, ukienda Pwani, utasema watu hawakulima. Lakini watu walilima, lakini hakuna mahindi kwa sababu yote yamesombwa na maji. Kwa nini na twalia hakuna maji? Twaweza kufanya kilimo cha unyunyizaji maji---"
}