GET /api/v0.1/hansard/entries/800341/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 800341,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800341/?format=api",
    "text_counter": 161,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Gona",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Twaweza kufanya kilimo cha kunyunyizia maji mimea, kwa sababu kwa vile mvua ni haba kule kwetu. Gavana aliyeko kule anayeona yale mambo, angehakikisha kwamba kuna mshiko fulani wa maji kuhakikisha kwamba maji hayo hayatafika kule kuwamaliza watu. Yatakikana majai yale yakingwe ili yasiwe yakifika kule ili wananchi wayatumie kwa kunyunyizia chakula. Hili ni jambo ambalo halifanyiki, na serikali ya kaunti na ya kitaifa zimekosa kushirikiana kwa ujumla katika jambo hili. Ni sisi ambao tunaangalia yanayofanyika, maanake tuko katika kaunti zetu kila siku. Mambo haya yanafanyika Kenya nzima; sio Nakuru, Kilifi ama Tana River peke yake. Yatakikana tuyaangalie haya mambo na tuwe na mfuatilio ili tufaulu. Hata mtoto kufanya vizuri, lazima kila siku uwe unaangalia vitabu vyake. Sasa sisi tukishapeana mwelekeo, tunaacha kabisa na hatuafuatilii tena. Lazima kuwe na mfuatilio, mshikamano na kusaidiana. Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono."
}