GET /api/v0.1/hansard/entries/800347/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 800347,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800347/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mwanzo kabisa, Bw. Naibu Spika, nataka nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nami pia nichangie Hoja hii, ambayo ni muhimu sana. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii na nataka nichukue nafasi hii ya kwanza kumshukuru Seneta wa Nakuru kwa msimamo aliouchukua tangu msiba huu uwakumbe watu wake. Twakushukuru kwa kusimama na watu wako, umekuwa sauti ya wanyonge. Kuna wengi ambao wamepinga msimamo wake lakini amesimama imara na sisi kama Seneti tutakuwa pamoja naye katika safari hiyo. Mwanzo kabisa, Seneta wa Nakuru alileta statement na wenzangu walichangia. Walipata nafasi ya kutuma rambirambi zao lakini mimi sikupata nafasi ya kufanya hivyo wakati huo kwa sababu sikuwa hapa ndani. Japo sikuwepo, nakuchukua nafasi hii kwa niaba yangu na kwa niaba ya familia yangu na watu wa Vihiga kusema pole kwa wale waliopoteza wapendwa wao na wale ambao mali yao iliharibiwa kutokana na mkasa uliowakumba. Huo ulikuwa mkasa mbaya sana. Namshukuru kwa sababu katika Hoja yake, kuna mambo manne ambayo Seneta wa Nakuru angependa kamati itakayoundwa itekeleze. Ni vyema tupate kiini cha kilichofanyika mpaka watu wetu wakapoteza maisha na mali yao kuharibiwa kama vile Sen. Kihika ametaja katika (a) ambapo amesema “holistically investigate”, just to quotewhat is in the Motion. Pili, tunataka haki kwa wale waliokumbwa na mkasa huo. Hiyo imejitokeza katika (b) ambapo amesema; propose modalities for compensation . Lazima wapate haki yao hata kama ni wanyonge na sisi kama Seneti tutasimama naye. Ya tatu ni ensure the dam owner makes compensation also na ya nne ni propose"
}