GET /api/v0.1/hansard/entries/800355/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 800355,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800355/?format=api",
"text_counter": 175,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mbali na majukumu ambayo Sen. Kihika ameorodhesha hapa, lazima waangalie jambo gani serikali zetu zote mbili zinaweza kufanya ili kukabiliana na majanga kwa sababu bado yatatokea. Hilo sio janga la mwisho kutukumba. Majanga bado yatatokea na lazima tuwe tayari kama serikali. Tusiwe tunategemea Shirika la Msalaba Mwekundu kutusaidia wakati wa majanga. Ndio maana nililetwa Hoja hapa tulipoanza Bunge la 12 kutaka sisi kama Serikali kutafuta njia ya kufadhili Shirika la Msalaba Mwekundu. Hoja hiyo ilipita lakini ningependa tuwe na Mswada kuangazia jinsi Serikali itaungana na Shirika la Msalaba Mwekundu ili shirika hilo lipate ufadhili kutoka kwa Serikali kwa sababu kazi wanayofanya ni kazi ambayo inafaa kufanywa na serikali zetu ambapo Wakenya wanalipa ushuru. Nilisimama ili kumhakikishia Sen. Kihika kwamba tuko pamoja naye na tuna imani na haya majina aliyopendeza. Hawa ni watu ambao tunawafahamu na amefanya mchanganyiko mzuri. Nina imani kuwa watafanya kazi tutakayowapa. Lazima mtu abebe msalaba wake. Kuna yule aliyesababisha yaliyotokea yakatokea na hatuwezi kuficha. Wanakamati hawa watakuwa na jukumu la kuchimbua ili tujue nani alisababisha vifo vya watu wetu. Tukishamjua, naye pia akabiliane na mkono wa sheria na Serikali iangalie jinsi ita-compensate watu walipatwa na mkasa huo. Asante sana Bw. Naibu Spika."
}