GET /api/v0.1/hansard/entries/800361/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 800361,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800361/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nilikuwa na hoja ya nidhamu wakati Sen. Khaniri alikuwa anazungumza lakini nakubaliana na vile ulisema. Wahenga walisema kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma. Alipoanza alikuwa na ari ya kuzungumza Kiswahili lakini akapata hitilafu baadaye. Kiswahili kinafaa kutukuzwa na Wakenya wamefurahia kwa sababu amejaribu. Naomba tutenge siku moja kwa wiki iwe siku ya Kiswahili ili Maseneta wote wajaribu kupata umaarufu wa kuzungumza Kiswahili."
}