GET /api/v0.1/hansard/entries/800918/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 800918,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800918/?format=api",
    "text_counter": 130,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ningependa kuangazia masuala mawili. Suala la kwanza ni kuhakikisha kuwa Wakenya wanakaa kama kitu kimoja. Mhe. Rais mwenyewe alitutangulia kwa kuomba msamaha kwa Wakenya wote ili watu wasameheane baada ya kutoka kwenye siasa ambayo ilikuwa kali na ya kivumbi mno. Alianza kwa kushikana mkono na kiongozi wa Upinzani mwezi wa Machi. Alipokuja hapa pia alisukuma mbele suala hilo kwa kulizungumzia na hivi majuzi kwa maombi ya kitaifa, vile vile aliangazia suala la umoja na undugu wetu na umuhimu wa Wakenya kuwa kitu kimoja na kujua maana ya msamaha."
}