GET /api/v0.1/hansard/entries/800919/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 800919,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/800919/?format=api",
    "text_counter": 131,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Jambo la pili ni kuhusu ugonjwa wa ufisadi. Mhe. Rais ameamua kukabiliana nalo. Hapo awali, alianza vita hivi lakini vikapata misukosuko hapo katikati. Lakini sasa inaonekana kuwa vita vimeshika kasi. Ni lazima tupigane na ugonjwa huu na tuushinde, la sivyo, utaangamiza Kenya. Hivyo basi naunga mkono Mhe. Rais kwa kazi nzuri anayofanya na vile vile kuhakikisha kuwa pesa ambazo zinazotumika zisifujwe ovyo ovyo. Naona ameingilia kwa upande wa wafanyakazi wa Serikali kuwa ni lazima wafanye kazi vile inavyotakikana haswa wale wanaohusika kwenye shughuli za kuhakikisha kuwa kandarasi zote zinazopeanwa katika idara mbali mbali tofauti za Serikali ziweze kufaidi wananchi."
}