GET /api/v0.1/hansard/entries/801305/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 801305,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/801305/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. King’ara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "Kiongozi wa nchi hakuacha nyuma magonjwa yanayotukumba. Kama vile mnakumbuka, alisema kwamba ugonjwa wa malaria ni janga ambalo lilikuwa linaumiza Wakenya sana. Serikali imechukua hatua na kuona hilo limepungua. Vile vile aliongea juu ya akina mama kujifungua bure. Alitaja kuwa kiasi cha Ksh5.2bilioni kilitumika na kitaendelea kutumika kuona akina mama wanajifungua bure. Hilo ni jambo la busara hasa kwa wanasiasa kwa sababu tunapenda wapiga kura. Kama hatushughulikii wapiga kura, basi tutaumia. Wakati afya ya wapiga kura inadumishwa ni jambo la kuvutia na kupewa kipaumbele."
}