GET /api/v0.1/hansard/entries/801360/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 801360,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/801360/?format=api",
"text_counter": 272,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Tandaza",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13287,
"legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
"slug": "kassim-sawa-tandaza"
},
"content": "Leo tulikuwa na mkutano na Mhe. Naibu Rais kule Kwale na tumeona bado wale walioko chini hawajakubali kwamba watu wanaweza kufanya kazi pamoja, ama wanaweza kuwa na maono pamoja na wakasaidia watu kwa kauli moja. Jambo lingine ambalo ningetaka kuchangia ni suala la viwanda. Ukweli ni kwamba nchi hii haitaweza kuendelea ikiwa viwanda havitanawiri. Kule kwetu Kaunti ya Kwale, kwa saa hii ndiko kuna madini ambayo yanachimbuliwa kwa wingi zaidi nchi nzima. Lakini la kushangaza ni kwamba katika karne hii bado tunachimbua yale madini na kuyapeleka Ulaya bila kuyafanyia kazi hapa. Hii inamaanisha faida kubwa haitufaidi sisi hapa nchini. Inamaanisha pia kazi ambazo zingetokea na kusaidia vijana wetu bado tunazipeleka Ulaya. Kwa hivyo, kuhusu viwanda ni lazima kuwe na mikakati maalum ya kuhakikisha kwamba sio tu kusema tutakuwa na viwanda wakati rasilmali zetu na mali ghafi bado tunapeleka katika nchi nyingine. Tuhakikishe usafishaji wa mali unafanyiwa hapa ili kuongeza faida na vijana wetu kupata ajira. Jambo lingine ambalo pia ni la msingi kwa viwanda ni bei ya kawi ilivyo hivi sasa. Ukweli ni kwamba katika nchi zote za Afrika Mashariki na Kati, Kenya ndiyo ina bei ya juu zaidi ya umeme. Huwezi kuzungumzia viwanda bila kugusia umeme. Ni jukumu la Serikali na washikadau wote, kuona kwamba kiwango cha bei ya umeme kimeregeshwa chini ikiwa ni kweli viwanda vinatakikana vinawiri. Mwisho ni suala ambalo kila kiongozi analizungumzia, ufisadi. Ukweli ni kwamba tuna tatizo. Mojawapo ya shida zetu ni mishahara ambayo wafanyajikazi wa Serikali wanapatiwa. Niliona tangazo wiki iliyopita kuhusu kazi fulani ya Serikali. Mtu anatakikana awe na shahada ya kwanza ama ya pili lakini mshahara wake wa kuanza kazi ni Ksh30,000. Ukweli usemewe. Je, mtu kama huyo ukimlipa Ksh30,000 unatarajia achunge mabilioni ya pesa? Hakika humtarajii atakuwa na maadili mema. Huwezi kumpatia fisi ambaye ana njaa nyama aibebe eti kwa sababu labda ni mcha Mungu ama umemwombea. Kwa hivyo, tukitaka kupambana na ufisadi ni lazima pia Serikali iwapatie wafanyakazi, hasa wale ambao wamesomea taaluma mbalimbali, mishahara ambayo itawasaidia. Kwa hayo machache, nakushukuru, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Pia natoa pongezi kwa Rais wetu kwa Hotuba yake aliyoitoa hivi karibuni."
}