GET /api/v0.1/hansard/entries/801465/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 801465,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/801465/?format=api",
"text_counter": 77,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Ahsante sana, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza ningependa kumshukuru Sen. Mercy Chebeni kwa kuleta Mswada huu. Wanuame ambao kazi yao ni kuwanajisi watoto sio wanaume, bali wao ni wanyama. Wanyama ni bora kuwashinda kwa sababu huweza kutofautisha kati ya watoto na watu wazima. Tabia za wanaume wanaofanya kazi hii imedorora. Mtu anapomnajisi mtoto, jambo la kwanza linalopaswa kufanywa ni kumpeleka katika hospitali inayoshughulikia walio na upungufu wa ubongo ili tuweze kuidhinisha kwamba vichwa vyao ni timamu. Tunaweza kuwa tunazungumzia watu ambao wako na akili punguani. Tabia hii inafanyika kote nchini kama vile Nairobi na maeneo mengine. Ni jambo la kusikitisha sana kusikia kwamba wanaume zaidi ya 21 wanamnajisi mtoto mmoja. Unashindwa ni nini walichokiona na kujivunia pale.Serikali inafaa kuwachukulia hatua kali. Sisi kama Bunge la Seneti, kazi yetu isiwe tu kuongea na kwenda nyumbani. Tunapaswa kufuatilia maneno ambayo tunayoyaongea hapa ili tuweze kujua chanzo cha matendo haya. Baada ya kujua, tuwachukulie hatua kali. Sio wazee wanaonajisiwa pekee, vijana wadogo pia wanalawitiwa. Tunapaswa kuwashughulikia pia, kwa sababu tukiwacha mambo yaendelee hivi, nchi yetu itapotea. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}