GET /api/v0.1/hansard/entries/801484/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 801484,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/801484/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Haji",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": "Bi. Spika wa muda, ningependa kumshukuru Sen. Mercy Chebeni. Kama vile jina lake ni “Mercy,” she is “merciful” ndipo akaleta Hoja hii hapa. Bi. Spika wa Muda, nafikiri nchi hii inataka maombi katika roho zetu sote. Mambo mengi yanaenda kombo kombo kwa sababu ya watu kutojali dini wala maadili ya jamii yetu ya Kiafrika. Sio wasichana peke yao wanaoharibiwa, bali pia wavulana. Kina mama pia wanajiharibu wenyewe kwa mambo ya usagaji; ilhali wanaume wanakubali kuoana wao kwa wao. Haya ni mambo yasiyoambatana na mila za Kiafrika wala dini yoyote ile. Kwa hivyo, kuna haja ya hatua kamili kuchukuliwa. Hawa wanaume wanaowaharibu hata vijana waliowazaa wenyewe sio watu wa kufungwa wala kufungwa maisha. Napendekeza kwamba watu hawa wanafaa kupigwa mawe mpaka wafe ili kila mtu aone kwamba kufanya mambo kama hayo ni hatia mbaya sana mbele ya Mungu na mbele ya nchi. Bi. Spika wa Muda, sidhani kwamba mambo haya yanaweza kutekelezwa na Wizara ya Elimu. Iwapo wazazi wenyewe hawafanyi wajibu wao, itakuwa vigumu kwa mambo kama haya kuisha. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono Hoja ya Sen. Mercy Chebeni. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}