GET /api/v0.1/hansard/entries/801930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 801930,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/801930/?format=api",
"text_counter": 269,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Makokha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2286,
"legal_name": "Geoffrey Makokha Odanga",
"slug": "geoffrey-makokha-odanga"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii kuungana na wenzangu ambao wametoa mashauri mema kuhusu Bajeti ambayo tumekuwa nayo. Ningependa kusema kwamba niko na masikitiko kidogo kwa sababa kama mwanakamati wa Kamati ya Kilimo, kuna mradi ambao tulikuwa tumekutana na tukakubaliana kwamba kwanza utafiti ufanyike kwa sababu mradi huu umekuwa ukipokea fedha kwa miaka kadha lakini mavuno yake hayalinganishwi na fedha ambazo zimekuwa zikipelekwa kwa mradi huu. Pili, ningependa kusisitiza kwamba ikiwa tutaenda na mpangilio wa Serikali wa kufanya nchi hii iwe ya kujitegemea kwa chakula, ni lazima katika Bajeti yetu pia tuweke fedha za kutosha kwa ukulima kulingana na mipangilio ya nchi za Afrika Mashariki na Kati. Ninasikitika kwa sababu kuna kampuni ambazo ziko katika chumba cha mahututi. Kampuni hizi ni kama Mumias, Nzoia, Muhoroni na Chemelil. Wakulima ambao wako katika sehemu hizi wanategemea ukulima wa miwa lakini katika Bajeti yetu hatujazingatia maneno ya ukulima wa miwa. Unapata kwamba kwa wakati huu sukari nyingi inatolewa kutoka nchi za nje. Kama tungeweza kuzingatia ukulima wa miwa katika nchi hii na tuweze kusaidia kampuni hizi kama Mumias, Nzoia, Muhoroni na Chemelil, tungekuwa na sukari ya kutosha katika nchi hii na kufanya hata wakulima wetu wawe na furaha na wawe na bidii ya kulima miwa. Jambo la tatu katika mipangilio ya Serikali ni kwamba kila nyumba itakapofika mwaka wa 2030 iwe na stima. Kuna mito ambayo haikauki. Iko na maji mwaka mzima. Mito hii inatoka sehemu ya Nyanza na Magharibi. Kama tungezingatia kujenga mabwawa ya kuzalisha umeme, hatungekuwa na shida ya upungufu wa hali ya stima. Kwa hivyo ninaonelea kuwa siku zijazo tuzingatie kuweka fedha na kuwa na mipango ya kujenga mabwawa katika mito hii ambayo haikauki kamwe."
}