GET /api/v0.1/hansard/entries/802866/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 802866,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/802866/?format=api",
"text_counter": 38,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Ahsante Bw.Spika. Nasimama kuunga mkono Taarifa hii kwa kusema ya kwamba nchi yangu ya Kenya ni nchi ambayo ni ya ajabu. Ni kama nchi ya kusadikika. Ukweli ni kwamba nikama tumeadhiriwa na ukoloni mamboleo kiasi cha kwamba hakuna kitu ambacho tunakithamini hapa nchini. Ni lazima tutafute kitu kinachotoka ughaibuni ndiposa tusema ya kwamba tunaendelea vizuri. Kwa hivyo, ukiona mambo kama haya yakitendeka, inaonekana ufisadi unakithiri. Kwa hivyo, nivizuri tujiamini kwanza. Inaonekana kwamba tunaendelea na ukoloni mamboleo. Tumepeleka fikira zetu na imani yetu yote ughaibuni. Kile ambacho tunafaa kufanya ni kujiamini. Nilienda Ujerumani na ndugu yangu Sen. Mutula Kilonzo Jnr. ambako kahawa ambayo imetoka hapa nchini inauzwa. Hiyo ndio kahawa ambayo ni nzuri sana. Tukienda huko, tunaaminika ilhali sisi wenyewe hatujiamini. Kwa wale ndugu zetu kutoka Zambia ambao wamekuja kujifunza mambo ya kupigana na ufisadi hapa Kenya, tunawakaribisha. Tutawafunza kwa sababu sisi wenyewe tumeona mambo hayo. Tukitilia mkazo ya kwamba tunataka kuwachana na hayo mambo, nina imani na ninajua ya kwamba tutaweza kufana. Lakini, itakuwa vigumu kama hatujiamini sana. Kamati ambayo itafuata mambo haya inafaa kupata chanzo na maana ya mambo haya kutendeka. Asante, Bw. Spika."
}