GET /api/v0.1/hansard/entries/802875/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 802875,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/802875/?format=api",
"text_counter": 47,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika. hivi karibuni tumeona kwamba, mhe. Rais baada ya kusalimiana kwa mkono na kupigana pambaja na mhe. Raila Amolo Odinga, waliipa kipaumbele swala la kupigana na ufisadi. Jambo hili la kutengeza mabasi laonekana limechukuliwa kabla ya Rais mwenyewe kuchukua hatua ya kupigana na ufisadi. Hivi sasa, kuna watu ambao kabla ya amri hii ya kupigana na ufisadi kikamilifu, wao walikuwa na mipango ya kuiba; walikuwa na mipango ya kufanya ufisadi ndani ya ofisi ili wapate pesa kutoka kwa umma. Ikiwa hili ndilo jambo ambalo walikuwa wanalidhania hawa wafisadi, basi nafikiria, mhe. Rais sasa hivi, ni wakati wake wa kuchukua nafasi hii kuweza kukomesha jambo hili. Katika nchi yetu ya Kenya, tuko na makampuni ambayo yanatengeneza mabasi. Mji wa Mombasa kuna Associated Vehicle Assembly wanatengeza mpaka malori, wacha mabasi. Ikiwa tunatengeza malori, sembuse mabasi? Tunao vijana wetu wa jua kali hapa Nairobi wanaopaka magari rangi, wanafanya repair na bodywork. Tuna makampuni kule Thika zinazotengeneza hata Land Rover. Sioni kwa sababu gani nchi yetu iingie hasara ya mamilioni ya pesa kama haya ya kuleta mabasi kumi, ishirini, thelathini au hamsini kutoka Afrika Kusini. Huu ni ufisadi. Tunamwomba mhe. Rais achukue hatua na kukomesha jambo hili ili lisitendeke tena. Kando na kutotendeka tena, mtu asiwe na fikira ya kufanya kitendo kama hiki ambacho wananchi wa Kenya watapoteza pesa kwa ajili ya ufisadi. Asante. Naunga mkono."
}