GET /api/v0.1/hansard/entries/802882/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 802882,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/802882/?format=api",
    "text_counter": 54,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, kupoteza mmoja katika familia ni jambo la kusikitisha, hasa ukizingatia kwamba Waislamu, wakatihuu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wamekuwa wakiitishwa vitambulisho au wanasimamishwa, wanawekwa pamoja na kupelekwa stesheni ya polisi saa kumi na mbili au saa moja za jioni. Hili ni jambo la kusikitisha. Pili, ikiwa mtu atashikwa na polisi, kunayosheria. Lazima afikishwe mahakamani amastesheni ya polisi, aandike s tatement, alale rumande ama aachiliwe iwapo hana uhalifu unaoweza kuleta tashwishi. Lakini tunaona kwamba mtu akishikwa sasa, anawekwa ndani halafu keshoye anapelekwa kortini na yale aliyoshikiwa nayo sio hiyo atakayoshtakiwa nayo. Ndio sababu tunaona mara nyingi polisi wanashika watu na baada ya kuachiliwa, wanaanza kesi zauongo, tena zakubandikiwa. Nitabia mbaya. Mwishowe, unapata kwamba polisi hawana kesi na wale watu wanaachiliwa. La kusikitisha ni kwamba mtu akiachiliwa, baadaye unampata amepigwa risasi na kuuawa. Wanasema eti huyo nijambazi aliyekomaa, kwa hivyo hakuna haja ya kumshika na kumfungulia mashtaka kortini; la kufanya ni kwenda kumchukua na kummaliza. Wazungu wanasema hii ni extra judicial killing . Sisi tunasema kwamba kitendo hiki sio haki. Askari akimshika mtu, basi lazima ampeleke kortini. Masuala haya sio kuhusu dini au kabila; bali kila Mkenya yuko na haki ya kulindwa na sheria, lakini hili jambo liko sana hapa nchini Kenya. Ingekuwa vizuri ikiwa polisi wataambiwa waache tabia kama hizi ili mtu yeyote akishikwa, wazingatie sheria za Kenya. Yule aliyeshikwa akipatikana na hatia, basi apewe adhabu kulingana na sheria. Lakini kuangamiza jamii katika familia sio jambo zuri hata kidogo. Asante sana, Bw. Spika."
}