GET /api/v0.1/hansard/entries/802889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 802889,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/802889/?format=api",
"text_counter": 61,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii kuweza kuchangia swala la polisi kubeba watu katika sehemu zao na kupotea. Hali si hali katika Kaunti ya Tana River. Polisi hubeba watu kwa magari ambayo hayana namba ya usajili. Hivi karibuni, vijana kwa majina Mohammed Ismael Somane, Jibril Abdi Somane walibebwa katika hali ya kutatanisha katika mji wa Hola. Watu ambao hawafahamiki walikuja na kuwabeba vijana hao na mpaka siku ya leo, vijana hao kutoka sehemu ya Bura hawapatikani. Magari yaliyowabeba yalikuja kwa hali ya kutatanisha. Wakati mtu wako anabebwa na watu wasiojulikana, utafanyanini? Huwezi kujua kama ni jambazi au polisi. Tumemaliza mwezi mzima na vijana hao hawajulikani mahali walipo. Familia zao ziko kwa hali ya majonzi kwa kuwapoteza vijana hawa. Hiyo ndiyo imekuwa maisha yao. Tunavyoona, watu kutoka jamii ya kiislamu ndio wanaobebwa. Tumelaani vikali jambo hili. Kwa wakati huu, imekuwa vigumu kwa watu kwenda Mskitini kuswali au kutembea usiku. Bw. Spika, vijana wengi hawataweza kutazama Kombe la Dunia kwa sababu wataulizwa kuonyeshana vitambulisho, waeleze wanakotoka na wanakoenda. Hali imekuwa ya kutatanisha katika sehemu zetu. Bw. Spika, kila mtu ana hakiya kuishi kama inavyo nakiliwa katika Kifungu26 (1) cha Katiba yetu. Sasa, hali yetu katika upande wa Pwani imekuwa ya kutatanisha. Vijana wetu wanatoweka na hatujui mahali wanakopelekwa. Mimi ningependa Seneti iweke Kamati ya kutafuta watu wetu kwa sababu hatujui mahali walipo. Mabibi na watoto wanalia na wamebaki bila baba. Katika hali hiyo, ningependa Kamati hii itafute watu wetu ili tujue mahali walipo. Kama waliobebwa wangepelekwa kortini, tungeenda kusikiza ili tujue ni sababu gani walishikwa. Lakini, kwa sasa, watu hawapelekwi kortini; wakibebwa wanaenda kabisa. Bw. Spika, katika maisha ya kiafrika, huwa tunaombea watu wetu tunapoona kaburi zao. Tunalaani vikali kwa sababu hatujaona kaburi za watu ambao walibebwa kwa hali ya kutatanisha. Polisi wa Kenya hawafanyi kazi nzuri. Wanavyofanya kazi haistahili kabisa. Sisi tunalaani kitendo hiki. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}