GET /api/v0.1/hansard/entries/802904/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 802904,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/802904/?format=api",
"text_counter": 76,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ambaye amefuga ndevu au nywele nyingi au mwenye asili ya Kisomali anachukuliwa kama gaidi. Vijana wengi sana wamepotea mtaani na inahuzunisha sana. Wazazi wengi wanalia na sisi vijana tunakosa mwelekeo. Inasikitisha sana kwa sababu polisi hawawezi kusema kuwa hicho ndicho chanzo cha kutumia mambo hayo kama mfumo wa uongozi. Vijana siku hizi mtaani wakiona “farasi mweupe” ambalo ndilo jina la gari aina ya Toyota Land Cruiser ya polisi, wanajua kuwa kwa mda wa mwezi au miwili hawataonekana mtaani. Naunga mkono Taarifa hii na kukemea matukio hayo. Pia, tunaomba idara za kijasusi na idara tofauti za polisi walegeze kamba lakini wasitumie mabavu kwa sababu hatutaendelea mbele. Kwa hayo machache, shukrani sana, Bw. Spika."
}