GET /api/v0.1/hansard/entries/803007/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 803007,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/803007/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bwana Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Mswada huu. Hususan Mswada huu unahusu pesa za uzeeni wakati mtu amestaafu. Ni jambo la muhimu kuwa na Shirika ambalo muajiriwa anaweza kuchanga pesa za kustaafu. Vile vile muajiri anafaa kulipa kiwango fulani kwa hazina hiyo. Katika muhula wa Seneti uliopita, nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kuangalia maswala ya wafanyikazi. Hata hivyo, kwa sababu mara nyingi sisi tuliegemea upande moja au mwingine, hatukupitisha Mswada huu katika muhula huo. Ilisikitisha kuona Wabunge wakiegemea pande mbali mbali. Sasa Mswada huu uko hapa na vile vile katika Bunge la Kitaifa. Mswada huu unahusu wafanyikazi wa serikali za kaunti. Bunge la Seneti liko na mamlaka ya kujadili Mswada huu. Kwa hivyo, kuna mvutano ambao ningeomba Spika wetu aongee na Spika wa Bunge la Kitaifa ili kuona kwamba Mswada huu umeachiwa Bunge la Senate ili tuweze kuujadili na kupitisha. Watu wengi hupata shida sana wanapostaafu. Wengine wanasafiri kutoka Mombasa, Kilifi, Kwale, Taita-Taveta na Busia hadi ofisi zilizoko Nairobi ili wapate pesa zao za kustaafu. Wao walichanga pesa hizo ili waweze kupata manufaa wakistaafu. Kadri tunavyo jadiliana, tunaimani kwamba Mswada huu ukipita, kutakuwa na shirika moja peke yake litakalo angalia mambo ya wafanyikaz ikatika kaunti zote 47 nchini. Kukiwa na shida ya kupitisha Mswada huu, kama vile nilivyo ona katika muhula uliokwisha, inafaa tujue kwamba wanaopata taabu ni wafanyikazi wanaofanya kazi katika zile kaunti. Hao ndio wanaokuwa na wasiwasi kwa sababu hawajui pesa zao zitakuwa namna gani, ama iwapo watazipata wakistaafu. Ni aibu kuona mtu mzima aliyefanya kazi kwa zaidi ya miaka 20, 30 ama 40 akihangaishwa kupata haki yake akistaafu. Kwa hivyo, nikiwa mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Wafanyi kazi, niko na imani kwamba Mswada huu utapitishwa ili kuhakikisha kwamba hawa wafanyi kazi wameshugulikiwa. Madhumuni ya Mswada huu ni kuwasaidia wafanyi kazi wa serikali za mashinani waweze kupata pesa zao watakapo staafu wakifika miaka 60 au wakati wanapofika miaka 50 ama 55 wanapotaka kuacha kazi wenyewe ama wanapopata kazi mahali pengine. Wanafaa kupata pesa zao ili waweze kupata haki zao na kuishi vizuri, sio kama wanavyoishi sasa wakistaafu. Bw. Naibu Spika, sijui kama kuna watu kama hao upande wa Meru, lakini ukienda Kilifi, utapata wamejaa. Mtu anaweza kushindwa kujua kama huyo mtu alifanya kazi ama alikuwa anatangatanga huku mjini peke yake, kwa sababu utamuona anapata shida. Hii ni kwa sababu hana cha kufanya wala hana malipo au maendeleo yoyote. Huyu mtu huwa amezeeka, ugonjwa na mateso yamempata mpaka utashindwa kujua kama huyu ndiye yule aliyekuwa akifanya kazi mjini na kuishi vizuri hapo awali. Haya yote hutokea kwa sababu ya kuchelewesha kupata malipo yake mtu anapostaafu. Utamwona mtu aliyestaafu akiwa na miaka 60 akianza kutafuta pesa zake mpaka afike miaka 70; anatafuta pesa zake kwa miaka mitano. Hii sio haki. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}