GET /api/v0.1/hansard/entries/803011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 803011,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/803011/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ama maono yao wenyewe. Hivi sasa, watu wameweza kukubaliana kuhusu mwelekeo wa hizi pesa mtu anapostaafu. Washikadau kama shirika la National SocialSecurity Fund (NSSF), Retirement Benefits Authority (RBA), Ministry of Finance – ama tunaiita Wizara ya Pesa – Trade Unions, ambayo ni mashirika ya kuwatetea wafanyikazi, na vile vile yale mashirika mawili yaliyo kuwa yakigombana zaidi ya County PensionFund (CPF) na Local Authority Pension Fund (LAPFUND). Washikadau wote hawa wameweza kukubaliana kuhusu mwelekeo wa pesa hizi ili mtu ajue kwamba akistaafu, atazipata namna gani. Niko na imani kwamba hawa wataweza kuangalia hizi pesa na kujua jinsi ya kuziweka. Jambo la mwisho, Bw. Naibu Spika, ningependa kuzungumzia juu ya wale watu ambao watajukumika kuangalia pesa hizi. Ni lazima tuangalie hawa ni watu wa aina gani. Hii ni kwa sababu tunaweza kuwaweka watu pale ndani, wawe wafisadi na wachukue pesa za wafanyi kazi, halafu wafanyi kazi washindwe kupata malipo yao. Kwa hivyo, natumaini kwamba jinsi Mswada huu ulivyoandikwa, lazima wale watu ambao watakaoongoza shirika hili wawe wamesoma na wako na uzoefu wa kuweka hizi pesa, ndipo mtu aweze kupata pesa zake anapostaafu. Nafikiria kwamba Mswada huu ukija wakati tutakapo usoma katika Third Reading, utaweza kuwa na manufaa zaidi na utaweza kuwasaidia wafanyi kazi. Asante, Bw. Naibu Spika."
}