GET /api/v0.1/hansard/entries/803031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 803031,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/803031/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wakati mwafaka kwa sababu awamu ya kwanza ya serikali za kaunti imekuwa na matatizo mengi hasa kwa wale wanaostaafu. Wafanyikazi walichukuliwa kutoka mabaraza ya miji iliyokuwepo hapo awali na wengi waliondoka bila malipo yoyote ya kustaafu kwa sababu kulikuwa hakuna mipango mwafaka ya kuwalipa wakati wanapoondoka. Niafurahi kwamba Mswada huu umewaleta pamoja washikadau wote wa sekta ya serikali za kaunti kuhakikisha kwamba wanana bodi ya kusimamia malipo ya uzeeni ya wafanyikazi wa serikali za kaunti. Vile vile, Mswada huu unatoa fursa ya kuchagua bodi huru ambayo haina ushawishi wa upande wowote. Ni kwa sababu ina wawakilishi kutoka kwa magavana, wafanyikazi, bodi ya wafanyikazi na wahusika wengine katika sekta ya serikali za kaunti. Bodi hii itakuwa na watu wenye tajriba kama vile shahada ya sheria, uhasibu, fedha na zinginezo ili kuhakikisha fedha zinalindwa bila kuporwa. Tatizo ni kwamba sheria inaweza kuwa nzuri lakini utekelezaji wake unakumbwa na misukosuko kadha wa kadha. Kwa mfano, lazima ufisadi uangaliwe kwa makini kwa sababu bodi nyingi kama hizi zina penyezwa na ufisadi kama tulivyoona Shirika la Malipo ya Kitaifa ya Uzeeni (NSSF) ambalo linasimamia wafanyikazi wengi nchini. Kwa hivyo, tungependa kuona kwamba sheria inayotungwa lazima ipewe fursa kutekelezwa na kuhakikisha kwamba wafanyikazi wanapata malimbikizi yao ya kustaafu bila matatizo yoyote. Tumeshuhudia wafanyikazi wa awamu ya kwanza ya Jumuia ya Afrika Mashariki ambao walistaafu miaka ya nyuma, hadi sasa hawaja lipwa ilhali wenzao katika nchini ya Tanzania na Uganda walilipwa mapato yao ya uzeeni na hawasumbuki wakitafuta mapato. Bw. Naibu wa Spika, sheria nyingi zinazotungwa katika Bunge zetu ni nzuri kwa ustawi wa nchi yetu. Hata hivyo, matatizo ni katika kutekeleza sheria hizo kuhakikisha wananchi wanapata usawa kutokana na vile ambavyo Bunge imeamua kutumikiwa. Hivyo basi, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu utasaidia pakubwa kuhakikisha wafanyikazi wa serikali za kaunti wanapata haki zao wanapostaafu."
}