GET /api/v0.1/hansard/entries/803839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 803839,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/803839/?format=api",
    "text_counter": 321,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chelule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13126,
        "legal_name": "Liza Chelule",
        "slug": "liza-chelule"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda kwa kunipa hii nafasi kuchangia mjadala wa mambo ya hesabu kuhusu ukulima wa samaki. Nimefurahia na nitafurahia ikipitishwa. Ingawa hivyo, pesa ambayo imepewa ukulima wa samaki ni kidogo sana. Hivyo nataka kusema kama Mbunge kwamba tutakapo tekeleza tena hesabu za mwaka ujao tuongeze pesa za kilimo cha samaki. Ninasema hivi kwa sababu ukulima wa samaki katika vidimbwi vya samaki umesaidia vijana na akina mama. Tunataka kujihusisha kama akina mama kwa mambo ya samaki. Kwa hivyo pesa ambayo imetengwa ni kidogo. Tukishughulikia masuala ya ukulima wa samaki baadaye, sharti tutenge pesa nyingi. Hii ni kwa sababu tutataka kujihusisha kama akina mama pamoja na vijana wetu. Ahsante sana."
}