GET /api/v0.1/hansard/entries/806841/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 806841,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/806841/?format=api",
    "text_counter": 51,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Lamu. Lamu kuna shule ambazo zimefungwa kwa sababu ya mambo ya kutokuwa na usalama. Wanafunzi wanapata shida kwa sababu wakiamka asubuhi, wanalazimika kuenda kutafuta maji walete kwa nyumba zao ili hayo maji yatumike kutengeneza chakula cha mchana na chakula cha usiku. Kwa hivyo, mpango huu utasaidia sana. Nikitoa ushuhuda, mimi ni mmoja wa waliofaidika na Maziwa ya Nyayo na tuliyafurahia sana. Matokeo yake yalionekana. Mpango huu ukifanyika utasaidia sana wanafunzi. Wabunge wakisema kila Mkenya anafaa kuwa sawa na Mkenya mwingine, bado tuna sehemu kama Lamu ambapo hatujakuwa sawa na wengine. Wale wanasema hivi labda wanaangalia Nairobi na kaunti zingine. Wanafaa wakienda Lamu wasiende Amu; waende Lamu Kaunti watembee. Wajua wengi wakija Lamu mjini wanaona ni tofauti na pengine watu wanajiweza. Kuna sehemu kama Basuba na Kiunga ambapo kuna matatizo mengi. Inabidi wanafunzi waende kwa hizo kambi za majeshi au askari ili wajipatie chakula hata cha kupeleka nyumbani. Lakini mpango huu ukiwekwa kwa shule, wanafunzi hawataenda kutafuta hivyo vyakula. Kwa hivyo, mpango huu ni mzuri sana. Tunaomba uwekewe mkazo ili usaidie wanafunzi wetu kwa shule. Pia, mpango huu utasababisha wale wana shida kwenda kusoma kwa sababu ya njaa kuja kwa wingi. Nina hakika mpango huu ukifanyika, hata baada ya miezi matatu, zile shule zitajaa wanafunzi. Mpaka sasa, kuna sehemu Lamu ambazo wanafunzi wengi hawaendi kusoma. Ukihesabu wale wametoka shule za msingi kuenda shule za upili, utaona kuna mwanya mkubwa. Tunapambana kama viongozi lakini matatizo bado yapo. Na ule mgao wa Lamu huwa ni kidogo; hauwezi kutusaidia. Tafadhali Wabunge, mkizungumza, wengine sisi matumbo yanatuuma mkisema Wakenya wengine ni sawa na wengine. Haijakuwa sawa. Tembeeni. Naomba mtembee muone sehemu kuna watu bado wanasoma chini ya miti. Kuna shule zimefungwa, wanafunzi wanabebwa kwa ndege kupelekwa shule za malazi ili wapate kusoma. Kwa hivyo, naunga mkono mpangilio huu sana. Naomba wenzangu wauunge mkono. Ni mpangilio wa maana sana. Ahsante."
}