GET /api/v0.1/hansard/entries/806993/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 806993,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/806993/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Mwanzo kabisa, tutaona mabadiliko katika magereza. Idadi ya vijana magerezani itapungua sana kwa sababu watakuwa wamepata jambo la kufanya. Lamu ni tofauti na kaunti nyingine kwa sababu kuna upande wa visiwa na ardhi, na matatizo yao ni tofauti. Katika Faza Ward, ambayo ni kisiwa kikubwa, vijana hupigana wakilipiza kisasi kwa sababu hawana kazi ya kufanya. Shule za michezo zikijengwa katika maeneo bunge, zitawasaidia pakubwa sana kwa sababu ni vijana ambao wanapenda kazi hiyo. Zitawafanya wawe na umoja na uwiano. Pia ikiwa hizo shule zitahusisha kaunti nzima, itabidi upande wa Lamu Mashariki na Lamu Magharibi waletwe pamoja ili wawe na uwiano."
}