GET /api/v0.1/hansard/entries/806994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 806994,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/806994/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Ndugu yangu, Woman Representative wa Isiolo, amesema kwamba kuna kaunti ambazo zina matatizo ya vijana kuvuka kwenda Somalia. Shule za michezo zitapunguza hilo tatizo pakubwa. Kumekuwa na matatizo mpaka akina mama wanalia kwa sababu hawajui ni nini kinachoendelea. Akina mama ambao wako nyumbani hawajui ukweli wakati watoto wao wanafuatwa na polisi. Haya matatizo yatakwisha vijana wakishiriki katika michezo. Pia, kuna tatizo la kuonea watu wengine wivu wakati wamekaa pamoja. Kuna wengine wamepata zaidi na wengine hawajapata. Wivu huchangia kuwepo kwa matatizo fulani katika Kaunti ya Lamu. Hali hiyo itapungua shule za michezo zikijengwa katika maeneo bunge. Watu wakiketi pamoja watapendana wakiona vile michezo inawasaidia. Hili ni jambo la maana sana, naomba liharakishwe kwa sababu, hakuna Mbunge ambaye atalikataa na kila mtu analipenda."
}