GET /api/v0.1/hansard/entries/808179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 808179,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/808179/?format=api",
    "text_counter": 108,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matungu, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Justus Makokha",
    "speaker": {
        "id": 13430,
        "legal_name": "Justus Murunga Makokha",
        "slug": "justus-murunga-makokha-2"
    },
    "content": " Ahsante sana Mhe. Spika. Lazima sisi kama Bunge tuchukulie hili jambo kwa njia inayotakikana. Ukiona jambo linaguza maisha ya mwanadamu, ni lazima sisi kama Wabunge tulichukulie hatua ambayo inatakikana. Maneno ya sukari yameongewa kwa muda mrefu katika nchi hii. Mimi kama Mbunge ambaye anatoka eneo ambalo linakuza miwa, wakulima wa miwa wanateseka. Kwa sasa, kiwanda cha Mumias kimekufa kwa sababu watu katika nchi hii wanatoa sukari nje kwa kiwango kikubwa hadi ile ambayo inatengenezwa katika viwanda vyetu haitumiki. Ya pili, unaona ya kwamba ripoti imetolewa jana na mahabara ya Serikali ya kuonyesha ya kwamba hiyo sukari iko na sumu. Ikiwa sisi kama Wabunge hatutachukua jambo hili kwa ile hali ambayo inatakikana, tutakuwa tunakosea nchi hii na wananchi wa Kenya. Kwa hivyo, nasihi Wabunge wote katika Bunge hili, ni lazima tuchukue hatua. Iwapo ni mimi ninahusika, nichukuliwe hatua ambayo inatakikana. Hatutaki kuonekana ya kwamba tunasaidia majangili wa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}