GET /api/v0.1/hansard/entries/808249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 808249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/808249/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Swala la ugavi wa pesa kwa sababu ya maswala ya ugatuzi linaguza Wakenya wote kwa sababu maana ya ugatuzi ni kupeleka maendeleo mashinani. Kazi inafanyika lakini kuna zile kaunti ambazo zimeweza kutumia hizo hera kisawasawa. Kuna zile ambazo zimeamua kufuja pesa. Isitoshe, pesa zile zinazochukuliwa kutoka kwa ushuru wa wafanyi biashara pamoja na zile zinatakikana kutumika kuwasaidia wananchi pale mashinani, zinachukuliwa na kufujwa vibaya sana. Kuna mchezo unaoendelea na sisi tunasema kutoka hili Bunge la kumi na mbili kwamba utukutu huu lazima ukome na pesa ambazo zinaenda kwa ugatuzi ziweze kutumika vizuri. Pia utakuta wameweka madai ya kandarasi ambazo ni gushi. Tunaomba pesa zitumike vizuri, na magavana hapa nchini waweze kusimamia hizi pesa za ugatuzi ili wananchi waweze kupata manufaa na faida. Naunga mkono."
}