GET /api/v0.1/hansard/entries/808336/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 808336,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/808336/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": {
"id": 13287,
"legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
"slug": "kassim-sawa-tandaza"
},
"content": " Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Mswada huu kwani ikija masuala ya bahati nasibu ni masuala ambayo yanaenda kinyume na maadili ya ufanyi kazi. Mambo ya bahati nasibu ni kwamba watu milioni moja wanachanga shilingi kumi kumi na inakuwa milioni mia moja lakini unachukua milioni moja unampatia mtu mmoja. Kwa kifupi bahati nasibu ni kama wizi. Unanyang’anya wengi mara milioni moja halafu unampatia mtu mmoja. Kwa hivyo, zingeongezwa kiasi cha kwamba watu wasiwe na moyo wa kufanya huu mchezo wa bahati nasibu. Kwa masuala ya utozaji ushuru, ningetaka kuchangia kwamba kuna wakati ambao vijana wengi waliambiwa kwamba wanahitajika wawe na PIN. Bila kujua, kwa hari ya kuwa labda wapatiwa mikopo na vitu kama hivyo, wakachukua PIN . La kushangaza, baada ya miaka mitano, ukitaka kuwasaidia hao vijana kwa kuwapatia kwa mfano zabuni, wakienda Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) kutafuta yale makaratasi yanahoyohitajika, wanaambiwa walipe faini takriban elfu sitini kwa sababu walichukua PIN lakini hawakufuatilia. Kama mtu yuko kijijini ni vigumu apeleke yale makaratasi yanayohitajika hata kama ni kila mwaka. Kwa hivyo, katika masuala ya utoaji wa ushuru na faini, ninaona kwamba mambo kama haya yangeangaliwa hasa kwa wale vijana ambao walipata PIN na hawajapata ajira yoyote wala hawajafanya biashara. Jambo lingine ambalo ningetaka kuongeza ni kuhusu hii Big Four Agenda za Mheshimiwa Rais. Mojawapo ni usambazaji wa nyumba ambazo zitaweza kufaidi wananchi. Hapo ningeomba ushuru kwa upande wa mbao zinazoletwa kutoka nchi za nje zizitozwe ushuru, ziziwekewe vyeti kwa sababu zikiwekewa hapa Kenya, tunajua kwamba tumepiga marufuku ukataji wa miti, naona moja kwa moja kutachangia ajenda isiweze kutimia ilhali ni ajenda ya manufaa kwa wananchi. La mwisho ni suala la madawa na ule ushuru ambao umewekwa. Tunajua kwamba mara nyingi, wale ambao wana pesa huenda India kwa matibabu. Lakini wananchi wengi hawana huo uwezo. Upande wa kule Pwani utakuta wengi wanategemea sana madaktari wa miti shamba. Utaona mtu anajiita daktari lakini huyu ni daktari wa miti shamba si daktari halisi. Hii ni kwa sababu ya bei ya madawa ambayo wengi hawawezi kujihimidi. Ikizidi, tunajua wengi kwa upande wa Pwani wanalazimika kuvuka mpaka kuenda nchi jirani ambayo matibabu iko chini. Kwa hivyo, moja kwa moja naunga mkono huu Mswada lakini kwa upande wa madawa na matibabu, lazima tuingalie upya. Hata tukisema tutapeana ule mradi wa kila mwananchi aweze kujisajili kwa NHIF, najua itachukua muda mrefu. Sioni kama mwananchi anastahili kuumia wakati tukingojea ile miradi ya Serikali ambayo itafuatilia. Kwa hayo machache, ninaunga mkono nikiongeza maoni ambayo nimetanguliza hapo mbeleni. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}