GET /api/v0.1/hansard/entries/808874/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 808874,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/808874/?format=api",
"text_counter": 54,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika. Lamu Kaunti imeathirika pakubwa na haya matatizo. Jambo hili limeleta shida sana. Kuna watu ambao nyumba zao zimevunjwa na maji. Kuna mama ambaye alitoka Chalaluma kuenda kujifungua hospitalini Witu, lakini kwa sababu ya kupanda kidau cha mbao kwa sababu pale Chalaluma kulikuwa kumezingirwa na maji, alijifungua ndani na mtoto akafariki. Kuna matatizo mengi Lamu Kaunti. Wenyeji ni maskini na kumetokea magonjwa mengi kama vile malaria. Tumepata msaada wa chakula lakini shida bado ni nyingi. Kuna wanyama ambao wamepotea. Mamba wanatembea na hata sisi wenyewe imebidi tuingie katika hiyo maji na mamba wako tele."
}