GET /api/v0.1/hansard/entries/809092/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 809092,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/809092/?format=api",
"text_counter": 272,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Wanyama",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru mwenzangu, Mhe. Muchira, kwa kuleta Hoja hii kuhusu watoto wetu ambao wamekwenda kwa huduma ya vijana, NYS. Ni kweli sisi hutoa watoto kutoka sehemu mbalimbali kuingia katika huduma hii kwa sababu tunataka pia wawe na pahali pa kukaa ama pa kufanya kazi. Vile mwenzangu amesema, wale wamehitimu wajiunge na kitengo cha usalama. Mimi ninaona hilo ni jambo muhimu sana. Sio tu kitengo cha usalama, hawa vijana wanaweza kujiunga na vitengo vingine vyovyote katika nchi yetu ya Kenya. Vile mwenzangu kutoka Isiolo amesema, ni kweli kuwa hapo awali walikuwa wanachukua watoto waliohitimu darasa la nane lakini mwishowe wakaanza kusajili waliohitimu kidato cha nne. Ni jambo nzuri iwapo sisi pia viongozi pamoja na Serikali tutasikizana kwa lengo moja na kusema kwamba vijana wetu wapewe kazi, sio kwenda kupata mafunzo na mwishowe warudi kukaa nyumbani. Kwa sababu kumekuwa na maneno mengi katika NYS na ninajua kwamba imekuwa changamoto na sio hapa tu kwa sababu wengi wanaongea kuhusu ufisadi. Ufisadi sio kwamba umelenga NYS pekee, umepatikana katika sehemu mbalimbali katika nchi yetu ya Kenya. Kama viongozi, tutasimama kidete kuhakikisha kwamba nchi yetu haitatumbukia mahali pabaya bali mahali pazuri. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}