GET /api/v0.1/hansard/entries/810240/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 810240,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/810240/?format=api",
    "text_counter": 634,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ninaunga mkono Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi ya kwamba Kipenglele cha 6 kiondolewe kwenye Ripoti hii kwa sababu Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi ijapokuwa kwa upande wao walijaribu kupigana na suala hili, hawakuwa na nguvu ya kusimamisha pesa sizipeanwe katika njia ile iliyotumika. Vile vile, sababu yangu nyingine ni kuwa suala hili la Tume ya Maadili na Kupambana dhidhi ya Ufisadi hapa nchini tumeibaidilisha mara nyingi kwa sababu hatujafurahia kazi ambayo imekuwa ikiendelea. Lakini Tume ya sasa imejaribu. Watu wakijaribu, tusiwapatie adhabu kwa kujaribu kazi ambayo wamefanya. Kwa hivyo, wakati tanapoendelea kuzungumzia Ripoti hii, itakuwa ni vizuri kulirudia tena jambo la pesa za mwananchi kutumika vizuri na kama hazijatumika vizuri, Kamati ifuatilie masuala hayo yote vilivyo."
}