GET /api/v0.1/hansard/entries/811491/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 811491,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/811491/?format=api",
"text_counter": 276,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante sana Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa Barabara, 2017. Mswada huu umekuja katika wakati mwafaka ambapo swala la barabara linazidi kuangaziwa katika Jamhuru yetu ya Kenya na pia kaunti zetu zote 47. Nitazungumza kuhusu Mombasa. Kwa muda mrefu sana Tumekuwa na barabara mbovu, hasa zile zinazounganisha Bandari ya Mombasa na nchi ya Kenya kwa ujumla. Mizigo nyingi inayotolewa Bandari ya Mombasa inasafirishwa kwa barabara ikielekea sehemu za bara ambapo inahitajika. Kwa muda mrefu sana barabara ya kuingia katika Bandari ya Mombasa ilikuwa mbovu na nyembamba sana kiasi ambacho magari miwili yenye mizingo hayangeweza kupishana. Lakini, nifuraha kuona kwamba barabara zote zinatengenezwa ikiwepo ile ya kutoka ndani ya bandari na kuingia barabara kuu ya Mombasa-Nairobi. Kuna barabara nyingine pia ambayo ilifunguliwa hivi majuzi na Mheshimiwa Rais ambayo inapitia Port Reitz na kuelekea mpaka Bonje. Hizi barabara zimetoa afueni kubwa kwa wakaazi wa Mombasa ambao wangetumia masaa matatu au manne kusafiri kutoka Mombasa Mjini hadi Mariakani. Barabara katika kivukio cha Causeway ambacho kinaunganisha Changamwe na Mji wa Mombasa pia kimepewa mwanakandarasi na kinarekebishwa hivi sasa. Hata hivyo, tunasikitika ya kwamba magari mikubwa bado yanatumia barabara hiyo na kusababisha msongamano na ajali nyingi katika sehemu hiyo. Ningependa kuzungumzia mambo matatu. Hivi majuzi tuliona taarifa katika vyombo vya habari iliyosema kwamba Mheshimiwa Waziri wa Barabara na Usafiri, Bw. Macharia, alisema kwamba wamefaulu kuyaondoa magarima mikubwa, hasa malori 500, barabarani kwa muda wa miezi sita ambayo Standard Gauge Railway (SGR) imeweza kuchukua makasha ya bidhaa kutoka Bandari ya Mombasa na kuyaleta Nairobi. Hilo ni jambo la kusikitisha kwa sababu wenye biashara ambao wanamiliki magari hayo hivi sasa wamepoteza biashara. Vile vile, wale watu ambao walikuwa wameajiriwa kufanya kazi kwenye hayo magari wamepoteza ajira. Vile vile, biashara katika baadhi ya miji kama Mariakani, Mazeras, Maungu, Voi na hata Mlolongo imepungua kwa sababu madereva walikuwa wakisimama katika vituo vile na kununua bidhaa tofauti tofauti. Waziri ameahidi kwamba kufikia mwisho wa mwaka, ataondoa magari elfu tatu hususan katika barabara ya Mombasa-Nairobi. Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu biashara ambayo inanpatikana kwa magari yale kutumia barabara ile itakwisha yote na miji mingi midogo midogo itakufa. Tumepewa mfano wa Mji wa Machinery, uliokuwa mji mkubwa wakati wa hapo nyuma, lakini sasa umekufa kabisa. Miji mingine mingi itakufa kwa sababu biashara itapungua kutokana na kulazimishwa kusafirisha makasha yanayo toka Bandari ya Mombasa kwa njia ya Standard Gauge Railway (SGR). Katika mpangilio huo, wananchi hawapewi fursa ya kuamua iwapo watasafirisha mizigo yao kwa magari au kwa SGR. Hili ni jambo la kusikitisha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}