GET /api/v0.1/hansard/entries/811495/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 811495,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/811495/?format=api",
"text_counter": 280,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "lakini wakachukulia kwamba ni sehemu ya barabara. Waliingilia watu alfajiri na kuwavunjia manyumba yao. Hili ni jambo la kusikitisha, kwa sababu wananchi wa Kenya wanataabika kwa mambo mengi. Kwa hivyo, wanapoweza kuimarisha biashara zao au kujenga makao yao, halafu yaje yavunjwe bila ya kulipwa ridhaa, jambo hilo linaweregesha nyuma. Ukienda huko, mpaka sasa utaona majumba mengi yamevunjwa katika barabara ya kuelekea Kilifi naupande wa Diani, katika Kaunti ya Kwale. Sio sawa kwa shirika la Kiserikali kama KeNHA, amabalo lina takikana kufuata sheria katika kufanya jambo kama hili. Iwapo wanataka kuvunjia watu majumba, wanafaa kutoa arifa ya kutosha. Pia wanafaa kuwatayari kulipa ridhaa iwapo ile sehemu wanayoichukuwa ni ya mtu binafsi. Bi. Spika wa Muda, jambo linguine nililo liona katika Mswada huu ni kwamba mashirika matatu yanatarajiwa kuanzishwa kusimamia mambo ya barabara. Hayo ni KeNHA, Kenya National Urban Roads Authority (KNURA) na Kenya NationalSecondary Roads Authority (KNSRA). Kwa vile sasa Serikali ni mbili; Serikali Kuu na serikali za ugatuzi, hakuna haja ya kuwa na mashirika matatu ya kusimamia barabara. Hii KNSRA haitakuwa na faida yoyote ikiwa kazi za barabara zitapewa serikali za kaunti. Hii itakuwa ni kulumbika mashirika wakati kazi zinazofanyika hazijulikani. Kwa hivyo, nakubaliana na mapendekezo ya wezangu ya kubadilisha jambo hili ilituwe na mashirika mawili tu; moja ya kusimamia barabara kuu,yaani KeNHA, na nyingine itakayo simamia barabara za kaunti katika Jamhuri yetu ya Kenya. Bi. Spikawa Muda, jambo la mwishoni kwamba, mara nyingi barabara za miji, yaani urban roads, zinaharibika haraka kwa sababu wanaopewa kandarasi za kuzitengeza hawana uzoefu. Mara nyingi, wanaopewa kandarasi zile ni kampuni zilizo andikishwa kuuza vitabu. Hatimaye, barabara zile zikijengwa, zinafukuka baada ya siku tatu au nne.Kwa mfano, hivi sasa Mombasa kunanyesha. Kuliponyesha juzi halafu kukakauka, barabara zilitengezwa. Hivi sasa kumenyesha tena na barabara zote zimefukuka, na imekuwa shida kwa magari kupita. Kwa hivyo, ni lazima kampuni zinazo pewa kandarasi za kutengeza barabara ziwe na uzoefu na ujuzi wa kufanya hizo kazi za kujeng barabara. La sivyo, barabara moja itakuwa inajengwa mara nne kwa mwaka, na tutakuwa tunapoteza raslimali chache za umma ambazo zinge tumika kwa masuala mengine. Kwa hayo mengi, Bi. Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa fursa hii. Asante."
}