GET /api/v0.1/hansard/entries/812140/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 812140,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/812140/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ningetaka kusikitika na wenzangu na kumpongenze sana Sen. Seneta kwa kuleta Hoja hii. Wengi ambao wako katika Soko la Gikomba si matajiri. Ni wanabiashara ndogo ndogo au watu wa tabaka ya chini kabisa. Moto unapotokea, mbali na kupoteza maisha ya mtu, hata yule aliyebaki hai ni sawa na yule aliyekufa. Hii ni kwa sababu anabaki hai lakini hajui kwa nini yuko hai. Kama ni mkopo alichukua kutoka kwa benki analipa polepole kutoka kwa mapato yake ya biashara yake ndogo. Moto unapotokea, yeye hupoteza Maisha, watoto wake, ndugu zake, marafiki na jamii yake. Na yeye mwenyewe anabaki akiwa na shida nyingi. Ni kama mtu aliyehai lakini ni mfu. Hana pesa ya kulipa mkopo wake. Umaskini unaendelea kuongezeka. Haya yote yanafanywa na wale wenye pesa. Kwa nini moto huu ulitokea Gikomba na si mahali pengine? Ninaashiria lawama zangu kwa usalama. Kuna mahali ambapo maofisa wa usalama wa hii nchi wanazembea. Maofisa hawa hawafanyi kazi yao inavyopaswa. Mara nyingi lawama zangu huziashiria vitengo vya usalama, hasa katika sehemu za Mombasa ambapo ninatoka mimi. Kuna moto unaowaka na kuuwa watu. Kuna moto mwingine ambao huwaka mioyoni. Kwa mfano, dawa za kulevya zimeingia nchini kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Ninaomba Kamati ya Bunge inayohusika na maswala haya ichunguze kwa makini upande wa usalama na nini kinachosabisha moto uwake kila wakati katika Soko la Gikomba."
}