GET /api/v0.1/hansard/entries/812147/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 812147,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/812147/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante sana. Ningependa kuunga hoja hii hususan kwa sababu tumeona watu wengi sana wakiuawa kiholela holela kwa mambo ambayo yamewadhuru yanayoweza kuzuiwa. Bw. Spika, imekuwa ni kana kwamba kila wakati tunaposikia wale wameuawa nitakwimu tu ambazo watu wanazisikia kuhusu mambo yanavyotendeka kwenye nchi hii ya Kenya. Hili ni jambo la kushangaza sana. Itakuwaje kwamba watu wametelekeza kazi yao, hivi kwamba umeme unaharibu mali, unaua watu, unaharibu biashara na watu wanakaa kana kwamba hatujui kiini cha mwanzo na hakuna mtu ambaye anachukuliwa hatua. Bw. Spika, juzi nimekuwa Malindi nikampata mwekezaji mmoja ambaye hoteli yake ilichomwa. Huyu ni mtu ambaye anasaidia wakenya kupata riziki ya kila siku. Tukiangazia utendakazi wa Kaunti hii yetu ya Nairobi, kuna mambo ambayo hayaridhishi hata kidogo, kwa sababu utakuta kwamba zima moto hazipo na wafanyikazi husika hawapo, ilhali pesa za Serikali zinatumiwa. Kila makadirio ya Serikali yanaonyesha kwamba lazima kuwe na mtu ambaye ni husika. Ninamuunga Mhe. Seneta kwamba lazima tuchukue hatua na hili Bunge lisikuwe tu ni Bunge la malumbano na gumzo lakini liweza kutoa kauli ambayo inaweza kuleta maaendeleo na mabadiliko ya maisha ya wakenya tunao watetea."
}