GET /api/v0.1/hansard/entries/812153/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 812153,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/812153/?format=api",
    "text_counter": 44,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ilioletwa na Sen. Mary Seneta. Kwanza, natuma rambirambi zangu kwa watu wa Nairobi, familia na wapendwa wa marehemu waliokufa kutokana na moto uliotokea wiki iliyopita. Huu sio mkasa wa kwanza wa moto katika eneo la Gikomba. Mikasa nyingi imepita lakini Serikali imelalia maskio na haki za Wakenya zinazidi kupotezwa kwa sababu ya moto. Ningependa pia kuchukuwa fursa hii kumueleza Sen. Mwaura kwamba kuna tofauti kati ya moto na umeme. Unapozungumzia moto anamaanisha ule unaochoma na kuunguza ilhali umeme unatumika kwa mambo mazuri. Kwa hivyo, moto na majanga kama haya yanayotokea hayapaswi kuchukuliwa hivi hivi. Mkasa wa moto kule Sinai haukushughulikiwa vipasavyo. Vile vile mkasa wa moto kule Gikomba uliotokea mwaka jana wakati wa kampeni pia haukushughulikiwa vilivyo. Kama itawezekena ile Kamati inayoshughulikia mkasa wa Solai inafaa kuongezewe majukumu ili tuhakikishe kwamba tumepata suluhisho kwa mambo kama haya. Moto ukitokea, wakenya wanakufa. Vile vile mafuriko yakitokea wakenya wanakufa. Kwa hivyo, haya ni mambo ambayo lazima tuyaangalie ili tupate suluhisho la kudumu kwa mikasa kama hii. Asante sana, Bw. Spika."
}