GET /api/v0.1/hansard/entries/812392/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 812392,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/812392/?format=api",
    "text_counter": 26,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana, Bwana Spika. Nataka kujumuika nawe pamoja na wenzangu kuwakaribisha wageni kutoka katika Kaunti za Busia na Trans Nzoia. Nawashukuru kwa sababu nilitembea katika Kaunti za Trans Nzoia na Busia, na niliona kuwa nyinyi ni watu wakarimu kabisa kwa sababu mulinikaribisha. Kwa hivyo, nami nachukua fursa hii kuwakaribisha hapa na kuwaambia kwamba sisi, kama Seneti, tumejitolea kutetea ugatuzi. Bw. Spika, kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi na Uhusiano wa Serikali, nawajulisha kwamba ugatuzi uko katika mioyo yetu; ni haki yetu kuutetea ugatuzi kikatiba na ni lazima tufanye kazi hiyo. Tutaweza kufanya kazi hii tukishirikiana nanyi, kwa sababu nyinyi ndio muko na uwezo pale mashinani kwa sababu mumepewa jukumu la kufanya kazi hiyo na Serikali. Kwa hivyo, nataka kuwahakikishia kwamba tutaifanya kazi hiyo.Tunawaomba na nyinyi pia mukiwa upande ule, muifanye kazi hiyo. Jambo linguine nililo sikia leo ni kwamba Sen. Sakaja alisema kuwa karibu asimame katika Kaunti ya Trans Nzoia. Lakini hayo ni maombi ambayo hayangefika mahali, kwa sababu najua angeshindwa na ndugu yangu, Sen. (Dr.) Mbito. Hii ni kwa sababu Sen. (Dr.) Mbito amekuwa akimualika huko, lakini sasa amesema anaweza kubadilisha nia yake, atembee huko na kusimamia kiti kule. Lakini kile kiti nitakacho mwambia asisimamie sio cha Useneta; pengine ajaribu kile cha Gavana, kwa sababu Gavana wa sasa atakuwa ameshatimiza awamu yake ya mwisho. Asante sana, Bw. Spika."
}