GET /api/v0.1/hansard/entries/812396/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 812396,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/812396/?format=api",
"text_counter": 30,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Asante, Bwana Spika kwa kunipa nafasi hii ili niwakaribishe waheshimiwa wenzangu kutoka Kaunti za Busia na Trans Nzoia. Nimesimama hapa kama mmoja wenu kwa sababu kuna wakati, kabla sijakuwa Seneta, nilikuwa mwakilishi wa wodi katika bunge la kaunti. Kwa hivyo, najua ni nini munacho pitia kule na pia changamoto munazo pitia. Bw. Spika, tegemeo la Seneti ni bunge za kaunti, hasa upande wa sheria na uwakilishaji.Wahenga walisema “dunia duara;” kwa hivyo sheria mnazo tunga hazifai ziwe za kuwapendeza nyinyi peke yenu, bali za kuwapendeza wananchi mnao wakilisha. Vile vile, naamini kwamba yule mwananchi wakawaida na wa chini kabisa ataangaliwa kupitia uwakilishaji wenu. Hii ni kwa sababu nyinyi ndio muko karibu na yule mgonjwa, na nyinyi ndio munaamka naye kila siku. Naamini kwamba sisi tunamjua mgonjwa, lakini nyinyi ndio munamjua vizuri zaidi kwa sababu nyinyi ndio muko naye. Kwa hivyo, tunawategemea sana kwa jambo hilo. Bw. Spika, nimetangulia kusema kwamba mimi ni mmoja wenu. Siku moja nilikuja Kaunti ya Busia kama mwanachama wa KADU Asili wakati huo ilikuwa aandikisha wanachama. Ukiniangalia bila ya kukwambia natoka wapi, utasema kuwa mimi ni mmoja wenu. Kwa hivyo, nashukuru kwa kuwa nilipata wanachama kule ambao walikuwa shida kuwapata awali. Lakini nilipotumwa upande huo, nilifanikiwa. Nilisema ni tumeni kwanza, nitawaangalia jinsi walivyo. Niliona kuwa mulikuwa watu makini mukizungumza, kwa sababu maneno mawili au matatu munayo zungumza, sisi Wapwani huwa twasikia munasema nini. Nashukuru na karibuni sana."
}