GET /api/v0.1/hansard/entries/812467/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 812467,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/812467/?format=api",
    "text_counter": 101,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Haji",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": "inayosema kuwa sehemu ambazo ziko nyuma zibakie nyuma maisha yote. Mpaka leo hakuna Serikali yoyote ambayo imejaribu kuinua maisha ya hawa watu. Kwa hivyo, hali imekuwa ya “nipishe nipate kuishi”. Wakati wa ukoloni wizi wa ng’ombe ulikuwepo lakini haukuwa kama vile ilivyo sasa. Watu wamejihami na silaha. Sehemu ambazo watu walikuwa wakipigana kwa fimbo, siku hizi wanatumia AK-47 au silaha kubwa kuliko hiyo. Nimekuwa nikizungumza na Sen. Sakaja. Tutawaita hawa watu pamoja lakini wajue kwamba sisi sio madaktari. Haya maneno yamezungumzwa tangu tupate uhuru na yanazidi kudorora kila siku. Kuna baadhi ya watu wanaoitwa homeguards, ambao wako na silaha. Hata hivyo, hizo silaha zinatumika kwa wizi na mauaji. Kama vile Sen. Wetangula alivyosema, wakati umefika ambapo Serikali inafaa kufikiria jamii yetu itawanywe katika sehemu mbali mbali nchini. Wengine wapelekwe Kakamega, Kisumu na kwingineko. Sehemu hiyo inafaa kutengewa utafiti wa mafuta na madini mengine. Kama sivyo, Serikali ichukue hatua ya kutwaa silaha na hata kutoa watu makende. Akina mama hawafanyi mambo hayo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}