GET /api/v0.1/hansard/entries/812476/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 812476,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/812476/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Haji",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": "Bw. Spika, nakushukuru kwa uongozi wako kwa sababu kiongozi lazima awe shupavu. Kila wakati matatizo yanapotokea anafaa kuwa na jawabu. Kwa hakika, haya maneno ni mazito sana kwa sababu watu wanauana kila siku na kuzidisha umasikini. Vile vile wakati Serikali inachukua hatua, watu wanaumia. Nimezungumza na mwenzangu hapa na tutajaribu. Lakini kutokana na experience yangu, maneno hayawezi kutatua matatizo. Kuna pesa zinazotengewa sehemu zilizotengwa kimaendeleo katika Katiba. Siku hizi hata Kibera imeongezwa katika kitengo hicho. Shida ya Kibera ililetwa na binadamu, hasa ukosefu wa mipango kamili. Shida ya wafugaji inatokana na maumbile ya Mungu. Jua ni kali na hakuna barabara na maji. Sasa hata hizo pesa kidogo zinazotengwa na Katiba, zimeanza kupeanwa kwa watu kule Kibera ilhali tunajua Nairobi iko na pesa nyingi kuliko kaunti zote. Kwa hayo machache, tutajaribu tuwezavyo."
}