GET /api/v0.1/hansard/entries/814335/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 814335,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/814335/?format=api",
"text_counter": 296,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi ya kuchangia. Naona huu ni Mswada mzuri ambao utasaidia sana. Pia, nakubaliana na Wabunge waliotangulia kuchangia kwamba kuna matatizo. Watu wengine wanakataa fidia ya shamba ambayo wanapewa na Serikali na wanasiasa wanaingilia. Kuna sehemu zingine ambazo ziko na matatizo zaidi. Watu wengine wanasema wamelipwa fidia kidogo ama wanataka Wabunge waingilie ili waseme walipwe vizuri. Sehemu zingine kuna matatizo, kwa mfano Lamu East. Kuna sehemu katika Kisiwa cha Pate ambazo hata Mhe. akienda anaona ni sawa. Mtu anaambiwa mnazi ukatwe alipwe Kshs3,000 na ataona ni dhuluma ya wazi. Utaona barabara ilikuwa gazetted mwaka wa 2007 na hapo kulikuwa na visima au kuna nyumba za miaka 200, kisha Serikali inawaambia wachukue Kshs3,000. Hii ni dhuluma."
}