GET /api/v0.1/hansard/entries/814336/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 814336,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/814336/?format=api",
"text_counter": 297,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Huu Mswada utasaidia katika Kaunti ya Lamu kwa sababu fidia itawekwa usawa. Katika sehemu zingine, gogo la stima linapita na watu wanalipwa Ksh500,000. Kisha mtu mwingine kwa hiyo Kaunti, analipwa Kshs3,000 na pengine umegawanya shamba lake. Limekuwa nusu na hawezi kuweka fence vizuri kwa sababu barabara imepita. Huu Mswada ukifuatwa vizuri utatusaidia sana. Utaleta usawa. Mara nyingine utaona majina yameandikwa na hayajulikani ni kina nani kwa sababu yamefichwa. Hawaweki uwazi. Unashangaa kwa nini haya majina hayawekwi wazi. Kuna tatizo gani. Huu Mswada unazungumzia mambo ya Internally Displaced Persons (IDPs). Itakuwa ni vizuri katika Kenya nzima tujue kwamba kuna sehemu zingine za Lamu ambazo kuna IDPs kutoka miaka ya nyuma wakati wa Shifta . Walifukuzwa kwao. Tukisikia IDPs, tunaona ni wa hapa bara, lakini kunao wa Pwani katika historia. Kuna watu wa bara ambao walifukuzwa kwao kwa sababu ya kukimbia mateso ya Shifta . Walikaa kisiwa cha Pate na wengine katika Lamu na Kilifi. Huu Mswada umeangazia mambo ya IDPs na itawasaidia. Lamu kuna IDPs."
}